Urushaji wa vijiwe kwa anayemuwakilisha mtu

Swali: Ni vipi mtu anarusha vijiwe kwa niaba ya mtu mwengine? Je, mtu anarusha kijiwe kimoja kwa ajili yake mwenyewe na kijiwe kingine juu ya yule asiyekuweko na kadhalika?

Jibu: Kwanza atarusha vijiwe saba kwa ajili yake mwenyewe. Kisha atarusha vijiwe saba vyengine kwa ajili ya yule anayewamukilisha. Hakuna neno akasimama mahali papo hapo wakati wa kurusha. Kwanza ataanza kurushia vijiwe kile kiguzo kidogo kwa ajili ya nafsi yake na yule anayemuwakilisha. Vivyo hivyo atarusha vijiwe kwa kile kilicho katikati na kile kiguzo kikubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (23) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 18/04/2020