Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya urafiki na ambaye anapuuza swalah?

Jibu: Haijuzu kufanya naye urafiki wala wengineo katika makafiri. Kwa sababu kuacha swalah ni ukafiri mkubwa kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni ijapo hatokanusha ulazima wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kati ya mtu na shirki na kufuru ni kuacha swalah.”

Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Ahadi ilipo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yeyote atakayeiacha basi amekufuru.”

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy na Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

Zipo dalili zingine zinazofahamisha hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/260)
  • Imechapishwa: 14/08/2022