Swali: Kipindi cha mwisho kumedhihiri baadhi ya vijana kusafiri kwenda nje ya Saudi Arabia na wanawaacha wake na watoto wao ambapo safari zao hizi ni pasi na haja. Ukiongezea kwa yale yanayopatikana kwa watoto katika katika kuwatelekeza na kupotea. Tunaomba nasaha na Allaah akujaze kheri.

Jibu: Kwa kweli jambo hili linasikitisha kwamba mtu anasafiri na anaiacha familia yake ilihali wao wanamuhitajia yeye katika matumizi, wanahitajia kuanasika naye, wanamuhitajia yeye katika maelekezo na malezi. Kisha anasafiri kwenda katika nchi ambayo huenda akapatwa na shari katika desturi, tabia na ´ibaadah zao.

Hivyo nawanasihi watu hawa wamche Allaah juu ya nafsi zao na wamche Allaah juu ya familia zao. Wabaki katika nchi zao. Wakitaka kusafiri basi wasafiri pamoja na familia zao kwenda Makkah, al-Madiynah na kwenginepo kwenye kheri na wao. Ama wao kwenda kuziteketeza nafsi zao na wakazitupilia mbali familia zao ni kosa. Ni upumbavu katika akili na upotevu katika dini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1476
  • Imechapishwa: 23/01/2020