Upindaji upi wa Qiblah unaomlazimu mtu kuzirudi swalah zake?

Swali: Kuna mgeni alifika Hunayzah kwa mara ya kwanza. Alikuwa akiswali swalah za faradhi msikitini ambapo yeye swalah za sunnah na mke wake swalah za faradhi wanaswali nyumbani. Hata hivyo baada ya siku nane walibainikiwa kwamba nyumbani wanaswali kinyume na Qiblah kwa sababu nyuma waliokuwa wanaishi ndani yake ilikuwa imepinda kiasi. Ni ipi hukumu ya swalah yake?

Jibu: Ikiwa kupinda kutoka katika Qiblah ni kidogo tu hakuna neno. Ama ikiwa amepinda sana kwa kiasi cha kwamba Qiblah akakipa mgongo, kuliani au kushotoni, basi ni lazima kwao kuzirudi swalah walizoswali. Ama upindaji mdogo haudhuru.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (56) http://binothaimeen.net/content/1283
  • Imechapishwa: 10/10/2019