Swali: Vipi kuhusu mwisho wa myahudi au mkristo ambaye hakusikia kuhusu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Mwisho wake anaachiwa Mola ambaye ni Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kuhusu sisi tunamzingatia kuwa ni kafiri. Kwa hiyo hatutomzika katika makaburi ya waislamu na watamsimamia makafiri wenzake. Kuhusu ataingia Peponi au Motoni anaachiwa Allaah (´Azza wa Jall). Yeye ndiye atasimamia hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (05) http://alfawzan.af.org.sa/node/2048
  • Imechapishwa: 26/11/2016