Upasuaji wa uzuri kwa ajili ya kuondosha kovu usoni

Swali: Miaka miwili iliyopita mtoto wangu wa kiume alianguka na akapatwa na kovu kwenye paji lake la uso. Kovu hili limekuwa likubwa. Je, inajuzu kufanya upasuaji wa uzuri ili kuondosha kovu hili?

Jibu: Ndio. Aende kwa madaktari na aangalie kama wanaweza kumtunza. Utunzaji ni jambo linalotakikana na zuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (68) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/27-06-1438h.mp3
  • Imechapishwa: 16/07/2017