Upande wa kulia na wa kushoto katika safu – upi bora?


Swali: Je, katikati ya safu ndio bora au upande wake wa kuume? Mahali ambapo wanawake wanaswalia watu wanamiminika kuunga safu upande wa kuume ama upande wa kushoto hakuna wanawake. Tunaomba utuwekee wazi hukumu.

Jibu: Hili ni kosa kukamilisha upande wa kuume na upande wa kushoto kusiwe na mtu. Upande wa kuume ndio bora zaidi ikiwa safu iko sawa au inakaribia kuwa sawa. Ama upande wa kuume kukiwa ni mbali basi kuwa karibu na imamu ndiko kunakuwa bora zaidi. Kwa hivyo tunasema upande wa kulia na wa kushoto unatakiwa kuwa sawasawa au ukaribiane. Hilo ni kutokana na faida mbili:

1- Kuwa karibu na imamu.

2- Imamu anakuwa kati na kati.

Sidhani kama kuna yeyote anayefikiria kuwa Maswahabah mmoja wao alikuwa anasimama nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wengine wanakamilisha upande wa kulia mpaka ujae, kisha ndio wanaanza upande wa kushoto. Sidhani kama hili lilitokea kwa Maswahabah. Kwa ajili hiyo wanachuoni wengi wametaja, akiwemo Ibn-ul-Muflih katika kitabu chake “al-Furuu´”:

“Wanaposema kwamba upande wa kuume ndio bora zaidi ni wakati safu inakaribiana kuwa sawa [na imamu] au iko sawasawa.”

Vinginevyo upande wa kushoto ukiwa karibu zaidi [na imamu] ndio bora zaiid kuliko upande wa kulia kukiwa ni mbali. Hili linahusu kwa wanaume na kwa wanawake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (52) http://binothaimeen.net/content/1184
  • Imechapishwa: 11/07/2019