Uongo mweusi na mweupe?


Swali: Inajuzu kusema uongo hali ya kufanya mzaha?

Jibu: Uongo haujuzu hali ya kutania wala kumaanisha kweli. Kwa sababu ni katika tabia mbaya ambazo hawasifiki nazo isipokuwa wanafiki tu. Miongono mwa mambo yanayokasirisha ni kwamba tunawasikia baadhi ya watu wanaugawanya uongo sehemu mbili; uongo mweupe na uongo mweusi. Ikiwa uongo unapelekea katika madhara kwa mfano kula mali, mashambulizi na mfano wa hayo, basi wanaonelea kuwa huu ndio uongo mweusi. Na kama ndani ya uongo hakuna mambo hayo, basi wanaonelea kuwa huu ndio uongo mweupe. Mgawanyo huu ni batili. Uongo wote ni mweusi. Lakini weusi unazidi kila ambavo utapelekea katika madhara makubwa zaidi.

Kwa mnasaba huu napenda kuwatahadharisha ndugu zangu waislamu kwa wanayofanya baadhi ya wajinga juu ya uongo wa April, na nadhani iko karibu. Uongo huu ambao wameuchukua kutoka kwa mayahudi, manaswara, waabudu moto na watu wa wengine wa kufuru. Isitoshe, pamoja na kwamba ni uongo, na uongo ni haramu Kishari´ah, na ni kujifananisha na wasiokuwa waislamu, na kujifananisha na wasiokuwa waislamu ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kujifananisha na watu, basi yeye ni katika wao.”

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Cheni ya wapokezi wake ni  nzuri. Dogo liwezalo kusemwa ni uharamu ingawa uinje wake wake unapelekea ukafiri kwa yule mwenye kujifananisha nao.”

Pamoja na kupatikana dhambi hizi mbili, kuna vilevile waislamu kujidhalilisha mbele ya maadui zao. Kwa kuwa ni jambo linalojulikana katika maumbile ya mwanadamu ya kwamba, yule mwigwaji hufurahia kwa yule mwenye kumwiga na huona kuwa yeye yuko mbele kuliko huyo mwengine. Kwa ajili hii ndio maana mwigaji amedhoofika mpaka akamwiga. Kwa hiyo muumini anajidhalilisha kwa kule kuwafuata kichwa mchunga makafiri.

Dhambi ya nne ni kwamba, mara nyingi uongo huu mchafu unapelekea kula mali za watu kwa njia ya batili na kuwatia khofu waislamu. Huenda akadanganya na kuwaambia watu wa nyumbani ya kwamba leo wana wageni na kwamba wawaandalie chakula kingi kukiwemo manyama na vinginevyo. Huenda vilevile wakawaambia jambo la kuwatia khofu, kama kwa mfano kuwaambia kuna ndugu ambaye kagongwa na gari na mfano wa hayo ambayo hayajuzu.

Ni lazima kwa muislamu amche Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), ajifakhari kwa dini yake na mwenye kupendezwa nayo ili maadui wa waislamu waweze kumuheshimu. Namdhamini kila yule ambaye atajitukuza kwa dini ya Allaah ya kwamba atakuwa mtukufu mbele ya watu na kwamba kila yule ambaye atajidhalilisha mbele ya maadui Zake atakuwa ni mdhalilifu na mdhalilifu; mbele ya Allaah na mbele ya maadui zake. Ee muislamu! Usidhani kuwa kule kuwafuata kwako makafiri na ukazichukua tabia zao kwamba eti watakutukuza ndani ya nafsi zao. Bali ni jambo litakutweza hali ya juu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (17) http://binothaimeen.net/content/6820
  • Imechapishwa: 16/03/2021