Swali: Tuna mwalimu katika lugha anayesema kuwa maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا

“… na atakapokuja Mola wako na Malaika safu kwa safu.”[1]

inaweza kufahamika upande wa lugha kuwa na maana ya kwamba amri ya Mola ndio itakayokuja na kwamba hatusemi hivo kama ´Aqiydah bali tunachokusudia ni kubainisha ni kiambatisho. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Amekosea. Ukisema “atapokuja Mola wako” maana yake ni kwamba “itapokuja amri ya Mola wako” umeisemea uongo lugha. Lugha inaposema kwamba fulani anakuja, basi yeye ndiye anayekuja. Wakati Aliposema (Ta´ala):

وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا

“… na takapokuja Mola wako na Malaika safu kwa safu.”

maana yake ni kwamba Yeye Mwenyewe ndiye atakayekuja na si amri Yake. Hayo aliyoyasema ni uongo juu ya lugha ya kiarabu. Haijuzu kumkubalia. Kile ninachojua kutoka katika chuo kikuu cha Muhammad bin Su´uud ni kwamba Ibn ´Aqiyl (Rahimahu Allaah) alithibitisha katika maelezo yake ya “Alfiyyah Ibn Maalik” na kwamba chuo kiliyawekea taaliki na kuwaamrisha waalimu kubainisha kuwa ni kosa.

[1] 89:22

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (9 B)
  • Imechapishwa: 13/07/2021