Uongo juu ya Ibn Baaz na Haatib bin Abiy Balt´ah


Swali: Wako watu wenye kusema kwamba Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) kabla ya kufa kwake alikuwa akifutu kwamba Haatib bin Abiy Balt´ah alikufuru kwa kitendo chake  na akiyaeneza hayo kati ya watu. Je, ni kweli kwamba Shaykh Ibn Baaz aliyasema hayo? Ni ipi hukumu ya kuyanakili na kuyaeneza?

Jibu: Allaah amemtakasa Shaykh Ibn Baaz kutokamana na maneno haya machafu. Huyu anamsemea uongo Shaykh Ibn Baaz. Sisi tulikuwa pamoja na Shaykh Ibn Baaz, tulifanya kazi pamoja naye na tukaketi naye mpaka katika pumzi zake za mwisho za kifo na hatukuwahi kusikia maneno haya. Shaykh Ibn Baaz hawezi kusema maneno kama haya. Kamwe! Lakini huyu ni mwongo na dajali. Mtu huyu hakuweza kumraddi baada ya Shaykh kufa, ndipo akaanza kumsemea uongo.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.ws/sites/default/files/bryhari--1427-10-28.mp3 Dakika: 1427-10-28/2006-11-20
  • Imechapishwa: 19/02/2021