Uombezi wa Mtume (صلى الله عليه وسلم) kwa ami yake ni maalum

Swali: Ni ipi maana ya uombezi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ami yake na Allaah (´Azza wa Jall) kumkubalia hilo?

Jibu: Uombezi huu ni maalum. Alimuombea lakini hata hivyo hakumkubalia na ndio maana Allaah akateremsha:

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ

“Haimpasi Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu… “[1]

Hapa ilikuwa ni kabla ya yeye kujua. Kisha baada ya hapo akaacha kumuombea. Amesema:

“Nitakuombea midhali sijakatazwa.”[2]

Alipokataza akaacha kumuombea.

[1] 09:113

[2] al-Bukhaariy (3884) na Muslim (24).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 05/07/2019