Uogaji wa Kishari´ah unamtosha mtu kutohitajia kutawadha?

Swali: Je, uogaji wa siku ya ijumaa, ´Iyd mbili na kuoga ili mtu upate baridi kidogo kunaangusha uwajibu wa kutawadha?

Jibu: Hapana. Uogaji uliowekwa katika Shari´ah ni kuoga siku ya ijumaa. Mtu mtu kuoga ili apate baridi kidogo uwepo wake ni sawa na kutokuwepo kwake; ni lazima iwe ni uogaji uliosuniwa.

Lakini mtu akioga kwa ajili ya ijumaa na wakati huohuo akanuia janaba kunamtosha. Lakini bora ni yeye kutawadha kabla ya hapo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/431/431.mp3
  • Imechapishwa: 09/07/2018