Swali: Jioni ya jana umesema kuwa haijuzu kununua dhahabu kwa kadi ya benki. Vipi kuhusu bidhaa zengine kama mabegi? Je, inajuzu kuvinunua kwa kadi ya benki?

Jibu: Haikushurutishwa ule uhamishaji wa pesa iwe mkono kwa mkono.  Uhamishaji wa pesa ni lazima iwe mkono kwa mkono pale ambapo mtu anafanya biashara kwa sarafu, dirhamu na dhahabu. Hapa ndipo kumeshurutishwa ule upeanaji wa pesa iwe mkono kwa mkono. Ama kununua bidhaa zengine kama kitambaa, matunda na kunde haikushurutishwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (69) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/12-07-1438i.mp3
  • Imechapishwa: 18/10/2017