Swali: Je, inajuzu kumuomba mwanachuoni mpwekeshaji duniani na kumwambia “Allaah akikuruzuku kukupa uombezi huko Aakhirah, basi nishufaie mbele ya Allaah.” Je, inajuzu kufanya hivi?

Jibu: Sijui msingi wa hizi Tawassul za Aakhirah kwa kusema “uniombee Aakhirah”. Badala ya kusema hivo mwombe hivi sasa akuombee. Ni kwa nini una haraka ya Aakhirah? Maadamu ni mtu mwema na wewe una haja ya du´aa, mwache akuombee hivi sasa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (01) http://alfawzan.af.org.sa/node/2104
  • Imechapishwa: 28/06/2020