Swali: Mwenye kukasirika na akatukana matusi mengi swawm yake inabatilika?

Jibu: Ni wajibu kwa muislamu kuuhifadhi ulimi wake kutokamana na kutukana na kuapiza siku zote na khaswa khaswa katika mwezi wa Ramadhaan. Kutukana sio katika tabia ya muislamu. Vilevile ni wajibu kwake kuvihifadhi viungo vyake kutokamana na kila kile alichokiharamisha Allaah. Akimtukana yeyote basi aseme:

إني امرؤ صائم

“Mimi nimefunga.”

Hivyo ndivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameufunza Ummah wake. Ikitokea akamtukana mwengine basi anapata dhambi. Swawm yake ni sahihi. Lakini inapungua thawabu kwa kiasi cha matusi yake kama yalivyo maasi mengine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule asiyeacha kusema uongo, kuutendea kazi na ujinga basi Allah hana haja yeye kuacha chakula na kinywaji chake.”[1]

Ameipokea Imaam al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.

[1] al-Bukhaariy (02/228) na matamshi ni yake, Ahmad (02/452-453), Abu Daawuud (02/767) na wengineo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/368-369)
  • Imechapishwa: 23/06/2017