Swali: Una nasaha zozote kwa wanawake juu ya kutumia fursa ya mwezi wa Ramadhaan?

Jibu: Mimi naona kuwa ni wajibu kwa walinganizi wa misikiti wawatahadharishe waislamu kutokamana na mfululizo wa maigizo na filamu hizi zinachochezwa mchana wa Ramadhaan ambazo wanazipa kichwa cha khabari kwa kuita ´filamu kadha` na ´michezo ya kuigiza fulani`.  Baadhi ya watu wanasema kuwa filamu hizi kunapatikana ndani yake mafunzo. Watahadharisheni juu ya haya. Hata kama kunapatikana ndani yake mafunzo Ramadhaan ni tukufu zaidi kuliko filamu na zinawapotezea muda wao. Tusemeje endapo zitakuwa ni filamu mbovu?

Ni wajibu kwa maimamu wa misikiti kuwatahadharisha watu kutokamana na jambo hili na kutokamana vilevile na mfululizo wa maigizo. Barnamiji hizi wanazokuwa nazo katika Ramadhaan huziandaa kwa muda mchache kabla ya Ramadhaan. Kwa sababu shaytwaan ndiye jeshi wa jambo hili. Jambo limezidi kuwa na shari zaidi. Ni wajibu kwa wahubiri wa misikiti kuwatahadharisha watu kutokamana na chaneli na intaneti hizi zilizojitokeza. Wana uwajibu mkubwa.

Kuhusu kinachotakikana kwa wanawake mchana wa Ramadhaan wanatakiwa kumcha Allaah katika Ramadhaan na miezi mingine. Lakini zaidi katika mwezi wa Ramadhaan kwa sababu hutoka wakaenda misikitini. Ni wajibu kwao kutoka hali ya kujisitiri. Ni wajibu kwao kutoka pasi na kujipamba. Hawatakiwi kujitia manukato wakati wa kutoka. Hawatakiwi kuchanganyikana na wanaume kwenye mabarabara, mitaa au kwenye milango. Anawajibika vilevile kuilinda nafsi yake kwa sababu ametoka kwa sababu ya ´ibaadah. Isiwe umuhimu wao ni kutaka kujipamba, kujipodoa, mashindano na ukereketwa kutaka kutazama mwanamke fulani amekuja akiwa hivi na mwanamke fulani ameenda akiwa hivi. Ni wajibu kwao kujiepusha na mambo haya na badala yake wajishughulishe na ´ibaadah na kumcha Allaah (´Azza wa Jall). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiwazuie wajakazi wa Allaah kutokamana na misikiti ya Allaah.”

Watoke hali ya kutojipamba, kujitia manukato na kuonyesha mapambo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaam al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14891
  • Imechapishwa: 09/06/2017