al-Halabiy amesema:

“Shaykh Ahmad an-Najmiy (Hafidhwahu Allaah) aliulizwa swali kama anapendekeza mtu kusoma ´Aqiydah kwa Mashaykh walioko Jordan wenye kusimamia “Markaz al-Albaaniy” na akajibu:

“Watu hawa wanahesabika kuwa ni Salafiyyuun, lakini umesema kuwa wanamsapoti na kumpendekeza Abul-Hasan na al-Maghraawiy. Mwenye kumpendekeza Takfiyriy kama al-Maghraawiy anahitajia kuangaliwa vizuri. Kwa ajili hiyo siwezi kusema mtu achukue elimu kutoka kwa mtu kama huyo.”

Hili si sahihi. Sisi tumekosoa makosa ya Abul-Hasan na ya al-Maghraawiy na kubainisha makosa yao…”

1- Ikiwa ni kweli ya kwamba mmewakemea pasi na kukubali nasaha, ni kwa nini hamkuweka makosa yao hadharani, kuwabainishia nayo watu na kujitenga mbali na wao?

2- Mpaka hii leo bado tunasikia jinsi Mashaykh wa Jordan wanavyotembelewa na watu wa Bid´ah kama Abul-Hasan al-Ma´ribiy na al-Maghraawiy. Mara nyingi huulizwa juu ya hilo na hapo husema kwamba ikiwa ni kweli kuwa ´Aliy bin Hasan al-Halabiy na Saliym al-Hilaaliy bado wanamsapoti Abul-Hasan al-Ma´ribiy na Muhammad bin ´Abdir-Rahmaan al-Maghraawiy, basi siwezi kusema kusomwe kwao. Kwa sababu tunasoma kwenye vitabu vya Salaf ya kwamba wamesema:

“Mwenye kumsapoti mzushi, akapata nasaha lakini asiipokei, akatwe kama anavyokatawa mzushi. Mtu asiwe naye kwa uzuri wala kuchukua elimu kutoka kwake.”[1]

Sikusema kitu kutoka kwangu mwenyewe. ´Abdullaah bin Muhammad adh-Dhwa´iyf amesema:

“Khawaarij wakaaji ndio Khawaarij wabaya zaidi.”

Ibn Battwah amepokea kupitia kwa al-A´mash ambaye amesema:

“Tulikuwa hatuulizii juu ya hali ya mtu baada ya kupata khabari ya mambo matatu; ni nani anayetembea naye, ni nani anayewatembelea na ni nani anayetangamana naye.”[2]

Amepokea kupitia kwa al-Awzaa´iy ambaye amesema:

“Endapo mtu atatuficha Bid´ah yake basi matangamano yake hayatofichikana.”[3]

Amepokea kupitia kwa Sa´iyd al-Qattwan ambaye amesema:

“Pindi Sufyaan ath-Thawriy alipofika Baswrah akaanza kuulizia juu ya ar-Rabiy´ bin Subayh na nafasi yake kwa watu. Akasema: “Ana I´tiqaad ipi?” Wakasema: “Hana I´tiqaad nyingine zaidi ya Sunnah.” Akasema: “Marafiki zake ni kina nani?” Wakasema: “Qadariyyah.” Ndipo akasema: “Basi na yeye ni Qadariy!”[4]

Ibn Battwah amesema:

“Allaah amrehemu Sufyaan ath-Thawriy. Amesema kweli, haki na kutokamana na elimu ya Qur-aan na Sunnah na hekima yenye kufahamika na wale wenye kuona na yanaeleweka kwa wajuzi.”

Dalili katika Qur-aan, Sunnah na matendo ya Salaf zinasema yule mwenye kuwatetea Ahl-ul-Bid´ah, kukaa pamoja nao, kuka na wao, kunywa na wao na kusafiri na wao kwa khiyari yake ni katika wao na khaswa pale ambapo tayari kishapata nasaha halafu baadae akaendelea na kitendo chake. Haijalishi kitu akisema kuwa kwamba anakaa nao kwa ajili ya kuwanasihi na khaswa si kwa mtu kama al-Maghraawiy ambaye wazi wazi amelemea katika Khawaarij.

3- Lau kama mngeliwakemea hadharani pasi na ya wao kupokea nasaha, basi ingelijulikana kama ambavyo inajulikana kuwa mnawasapoti na kuridhika nao.

[1] Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 271, cha Abu Daawuud.

[2] al-Ibaanah (419).

[3] al-Ibaanah (420).

[4] al-Ibaanah (421).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Durar an-Najmiyyah fiy Radd-ish-Shubuhaat al-´Aqadiyyah wal-Manhajiyyah, uk. 371-374
  • Imechapishwa: 18/03/2017