´Umrah ya Mtume (´alayhis-Salaam) katika Rajab


Swali: Je, imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba alifanya ´Umrah katika mwezi wa Rajab?

Jibu: Kinachotambulika kwa wanachuoni ni kwamba hakufanya ´Umrah katika mwezi wa Rajab. Bali (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya ´Umrah katika Dhul-Qa´adah. Imethibiti kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya ´Umrah katika Rajab[1]. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema ya kwamba alikosea katika hilo na akaweka wazi ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakufanya ´Umrah katika Rajab. Kanuni ya msingi inasema kuwa mthibitishaji anatangulizwa kabla ya mkanushaji. Huenda ´Aaishah na wale wenye kuonelea maoni yake hawakuhifadhi yale yaliyohifadhiwa na Ibn ´Umar.

[1] Tazama http://firqatunnajia.com/kufanya-ibaadah-maalum-mbalimbali-katika-rajab/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alifta.net/Fatawa/FatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=341&PageNo=1&BookID=12
  • Imechapishwa: 22/03/2018