Swali: Wanazuoni wengi wanaona kuwa kufanya ´Umrah katika mwezi wa Rajab ni Bid´ah. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Hakuna neno kufanya hivo. Salaf walikuwa wakifanya hivo, kama alivotaja Ibn Rajab. ´Umar na wengineo walikuwa wakifanya ´Umrah katika Rajab. Imesihi kutoka kwa Ibn ´Umar kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya ´Umrah katika Rajab.

Swali: Vipi kuhusu kufanya ´Umrah katika masiku ya hajj au mwezi wa hajj?

Jibu: Afanye hivo. Kuna fadhilah kufanya ´Umrah katika Dhul-Qa´dah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya ´Umrah katika Ramadhaan na vivyo hivyo kunalingana na kuhiji. Lakini mtu anafanya ´Umrah katika kila wakati. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”`Umrah moja hadi nyingine ni kifutio cha madhambi kwa yaliyo baina yake na hajj yenye kukubaliwa haina malipo mengine isipokuwa Pepo.”

Mwaka mzima ni wakati wa kufanya ´Umrah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21570/حكم-العمرة-في-شهر-رجب-واشهر-الحج
  • Imechapishwa: 25/08/2022