´Umrah au I´tikaaf katika Ramadhaan?

Swali: Ni kipi bora ´Umrah katika Ramadhaan au kufanya I´tikaaf?

Jibu: Kufanya ´Umrah katika Ramadhaan hakupingani na I´tikaaf kabisa. Kwa sababu I´tikaaf inakuwa katika zile siku kumi za mwisho na ´Umrah inakuwa katika kila mwezi. Anaweza kufanya ´Umrah mwanzoni mwa mwezi na akajitolea kufanya I´tikaaf.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1566
  • Imechapishwa: 03/03/2020