Umbali wa 150 km baina ya nyumbani na kazini

Swali: Sisi ni kundi la waalimu ambao tunaishi mbali na masomo zaidi ya kilomita mia moja na khamsini. Tunaenda kila siku katika masomo hayo. Tumetofautiana kuhusu hukumu ya kufupisha na kukusanya inapokuja katika swalah ya Dhuhr na ´Aswr. Je, tuna haki ya kufupisha na kukusanya kutokana na umbali huu ilihali tunaenda kila siku katika masomo hayo?

Jibu: Lililo salama zaidi ni nyinyi kutofupisha wala kukusanya. Kwa sababu  mfano wa mwendo kama huu watu hawazingatii kuwa ni safari japokuwa baadhi ya wanachuoni kweli wanaona kuwa ni safari. Ninavyoona ni kwamba wasikusanya wala wasifupishe. Iwapo tutakadiria kuwa wamefika kwa familia zao na wamefika hali ya kuchoka na wanachelea wakilala hawatoamka isipokuwa wakati jua limekwishazama au wanachelea wakisubiri ´Aswr watakuwa katika hali ya kupiga miayo, katika hali hii tunawaambia wakusanye. Kwa sababu kukusanya ni jambo pana zaidi kuliko kufupisha. Katika hali hii ni sawa wakakusanya. Watapofika katika nchi yao wanalala mpaka wakati wa kuzama kwa jua. Ama kusema kufupisha naona kuwa lililo salama zaidi wasifupishe. Kwa sababu hii haihesabiki kuwa ni safari katika desturi ya watu hii leo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (60) http://binothaimeen.net/content/1366
  • Imechapishwa: 24/11/2019