´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) na Nisfu Sha´baan

Swali: Kuna mapote ambayo yanasherehekea usiku wa Nisfu Sha´baan na wanasema kuwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akisherehekea usiku huu. Tunaomba utubainishie hukumu?

Jibu: Wanamsemea uongo ´Umar. ´Umar hakuwa anafanya hivi. ´Umar ni miongoni mwa watu waliokuwa msitari wa mbele kabisa kujitenga mbali na Bid´ah na kutahadharisha nazo. Usiku wa Nisfu Sha´baan hakukuthibiti kitu na tarehe 15 Sha´baan hakuna swawm. Hili halikuthibiti. Hii ni miongoni mwa Bid´ah ambazo Allaah hakuteremsha dalili yoyote juu yake.

Mwenye kutaka kufanya ´ibaadah ashikamane na mambo yaliyowekwa katika Shari´ah na yale yaliyowekwa na Allaah na Mtume Wake. Haya yatamtosheleza na Bid´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14005
  • Imechapishwa: 19/04/2018