´Umar bin ´Abdil-´Aziyz khaliyfah mwongofu wa tano?

Swali: Mwenye kumwita ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz khaliyfah mwongofu wa tano licha ya kwamba Mu´aawiyah…

Jibu: Baadhi yao husema hivo. Yeye – Allaah akitaka – ni khaliyfah mwongofu. Lakini makhaliyfah waongofu kikweli ni wanne. Lakini yeye pia ni khaliyfah mwongofu. Kila kiongozi mwema anaitwa khaliyfah mwongofu.

Swali: Wanazuoni wamekubaliana juu ya kwamba Mu´aawiyah ni mbora kuliko yeye?

Jibu: Mu´aawiyah yeye ni Swahabah. Mu´aawiyah ni mbora kuliko yeye. Yeye ni miongoni mwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21528حكم-وصف-خليفة-راشد-لعمر-بن-عبدالعزيز
  • Imechapishwa: 23/08/2022