Swali: Nilioa mwanamke nikabaki nae kwa muda, kisha nikamtaliki na akaolewa na mwanaume mwingine baada yangu. Je, inajuzu kwake kumbusu na kumsalimia baba yangu baadaya kumtaliki?

Ibn Baaz: Hakuna ubaya. Kwa kuwa Allaah Kasema:

وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ

“Na (mmeharamishwa) wake wa watoto wenu.” (04:23)

Ni katika wake wa watoto (walioharamishwa kwa baba). Hata kama amemtaliki. Ni Mahram wa baba yako.

Muulizaji: Yaani umahram wao ni wenye kubaki hata kama amemtaliki?

Ibn Baaz: Ni kama mke wa baba yake, lau baba yake atamtaliki, bado (mama huyo) ataendelea kuwa Mahram wake (mtoto). Allaah Kasema:

وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ

“Na wala msiwaoe (wake) waliowaoa baba zenu.” (04:22)

Baba akimtaliki (mke wake) au mtoto (mke wake), anakuwa ni Haraam (huyu kwa yule, na yule kwa huyu).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb (770)
  • Imechapishwa: 10/03/2018