Ulazima wa mzushi kubainisha hadharani Bid´ah yake baada ya kutubia

Swali: Kuna mtu alianzisha katika Uislamu mwenendo mbaya kisha akatubia. Lakini wafuasi wake hawakutubia kutokamana nao. Je, anapata dhambi ya hilo na dhambi za wale wafuasi baada ya kutubia kwake?

Jibu: Udhahiri ni kwamba hapati dhambi yoyote. Kwa sababu mtu huyu ametubia. Akitubia Allaah anasamehe kila chenye kuhusiana na dhambi hii. Kutokana na swali la muulizaji huyu inapata kutubainikia ukhatari wa Bid´ah. Mtu akianzisha Bid´ah ovu – itambulike kuwa kila Bid´ah ni upotevu – na watu wakaifanya kuwa ni Sunnah, wanakuwa ni wenye kuhuisha Bid´ah hii kwa kujengea kitendo chake yeye – tunaomba ulinzi kwa Allaah.  Matokeo  yake anapata dhambi zao. Lakini akitubu udhahiri wa maandiko yanaonyesha kuwa yule mwenye kutubia kutokamana na dhambi ni kama ambaye hana dhambi. Miongoni mwa masharti ya tawbah ni lazima vilevile abainishe kuwa amejirudi kutokamana na Bid´ah zake na badala yake amefuata njia sahihi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/823
  • Imechapishwa: 02/03/2018