Ulazima kwa bosi kufanya uadilifu kati ya mfanyakazi muislamu na kafiri


Swali: Mimi nina wafanyakazi wawili ambapo mmoja wao ni muislamu na mwengine ni kafiri. Wote wawili wako sawa katika kazi. Linalonipasa mimi ni kufanya uadilifu kati yao. Je, inajuzu kwangu kumfupizia kafiri haki yake kwa sababu ya dini yake?

Jibu: Kilicho cha wajibu ni wewe kufanya uadilifu kati yao. Lakini ni lazima kuwaweka mbali makafiri hata kama ni wachangamfu zaidi [kazini]. Kwa sababu muislamu ni mwenye baraka zaidi ijapokuwa ni mwenye ufanisi mdogo kuliko. Tusemeje wakiwa wako sawa. Imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba aliacha anausia kuwaondosha makafiri nje ya kisiwa hiki na kwamba kusibaki dini mbili[1].

[1] Tazama http://firqatunnajia.com/63-makatazo-ya-kuwaacha-makafiri-wakamakinika-na-kutanua-katika-kisiwa-cha-kiarabu/ 

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/380) https://binbaz.org.sa/fatwas/924/%D9%88%D8%AC%D9%88%D8%A8-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D8%AF%D9%84-%D8%A8%D9%8A%D9%86-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D8%A7%D9%85%D9%84-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B3%D9%84%D9%85-%D9%88%D8%BA%D9%8A%D8%B1%D9%87
  • Imechapishwa: 09/12/2019