Ukweli kuhusu wazazi wake Mtume (صلى الله عليه وسلم)


Swali: Baba na mama yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wako Peponi au Motoni?

Jibu: Baba na mama yake walikuwa katika kipindi cha kikafiri. Walikufa katika kipindi cha kikafiri. Imepokelewa katika Hadiyth:

“Hakika baba yangu na baba yako wako Motoni.”[1]

Alimuomba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Mola Wake amuombee msamaha hakupewa idhini. Kwa sababu alikufa katika kipindi cha kikafiri na juu ya dini ya watu wake ambayo ilikuwa ni kuabudu masanamu.

Swali: Je, mama yake si katika Ahl-ul-Fatrah?

Jibu: Udhahiri wa Hadiyth zinaonyesha kuwa ni miongoni mwa watu wa Motoni. Kwa sababu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliomba ruhusa amuombee msamaha lakini hakupewa ruhusa hiyo. Kuna uwezekano vilevile ikawa ni miongoni mwa Ahl-ul-Fatrah. Lakini imekuja katika baadhi ya mapokezi kwamba ni miongoni mwa watu wa Motoni kama mfano wa:

“Hakika baba yangu na baba yako wako Motoni.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Swali: Je, walifikiwa na baadhi ya kitu katika mafunzo ya dini zilizotangulia?

Jibu: Pengine alifikiwa na khabari za dini ya Ibraahiym (´alayhis-Salaam), mambo ambayo yalifanya hoja kumsimamia.

Swali: Ibn Hishaam ametaja kwamba aliingia katika Uislamu. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Hili halina msingi. Mwenye kusema kwamba baba na mama yake walisilimu ni khabari za batili.

[1] Muslim (203).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 66-67
  • Imechapishwa: 08/07/2019