Ukweli Kuhusu ISIS na an-Nusrah


Swali: Kuna vijana wa hamasa wameenda Syria na wamejiunga na kundi linalojiita “dola ya Kiislamu”. Wanasema kuwa tuhuma za kwamba wanaua na za ugaidi si kweli. Ni upi ukweli juu ya kundi hili?
Jibu: Ukweli ni kwamba ni Khawaarij na Takfiyriyyuun. Siku chache zilizopita wamemuua mtoto wa binamu yangu. Wamesema kuwa ameritadi kwa kuwa alikuwa upande mwingine wa jeshi la wapinzani. Majeshi yote mawili ni wapotevu. Haijalishi kitu sawa ikiwa wanaitwa an-Nusrah au ISIS. Hata hivyo hili la mwisho ni baya zaidi hata kama yote mawili hayawasalimishi waumini. Kuthibitisha upuuzi wao inatosheleza kwa siku chache zilizopita kutangaza kwao Khaliyfah ambaye wanadai kuwa ni Khaliyfah wa Waislamu. Kitu cha kwanza wanachofanya na raia wetu wanaojiunga nao ni kuchukua kiapo cha utiifu na usikivu (bay´ah) kutoka kwao. Mnajua ni vipi hukumu ya kuchukua kiapo cha utiifu na usikivu inavyokuwa. Sisi sote tunaishi chini ya kiapo cha utiifu na usikivu. Mnaishi chini ya kiapo cha utiifu na usikivu cha mtawala wa nchi hii. Hii ni khiyana na usaliti. Siku ya Qiyaamah bendera ya wasaliti itanyanyuliwa ambayo itakuwa imeandikwa “Huu ni usaliti wa fulani”. Yule mwenye kujichukulisha bay´ah basi yuko katika khatari. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuacha Jamaa´ah kiasi cha Shibr[1] na akafa, basi amekufa kicho cha Jaahiliyyah.”

“Yule mwenye kunyanyua mkono kutoka katika utiifu atakutana na Allaah pasina kuwa na hoja yoyote.”

Watu hawa wanavunja mkataba. Wako mbali kabisa na haki. Wanawakufurisha wanachuoni wetu na watawala wetu. Hamu yao kubwa ni Takfiyr. Hilo ndilo walijualo na ndilo wanaloitakidi kuwa ni Dini. Wamedanganyika na fataawa ambazo zinawatolea wapumbavu walioko nyuma ya pazia. Wako sampuli mbili:

1- Wale wanaowatolea fatwa na wako pamoja na wao. Wamewafanya kuwa ni wanachuoni wao. Wameambatana nao na hawarejei katika hukumu ya Allaah na hawarejei kwa wanachuoni Rabbaaniyyuun.[2] Watu hawa ni kama wao.

2- Wale wenye kukaa chini na kutoa fatwa. Huenda wakawa katika miji yetu na kuwapa fatwa. Wanawasapoti na kuwapa moyo watu kwenda katika boli hii inayowaunguza vijana wa Kiislamu pasina malengo. Wanapigana vita chini ya uongozi wa upofu, ukabila na unaoafikiana na wakati wa kikafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si katika sisi yule anayepigana chini ya uongozi wa upofu, ukabila au analingania katika uongozi wa ukabila.”

Watu hawa ni wajinga, wendawazimu, vijana na wapumbavu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametahadharisha nao na kusema:

“Lau nitakutana nao basi nitawaua kama jinsi walivyouawa kina ´Aad.”

Amesema pia muuaji bora ni yule mwenye kuwaua na kwamba wauliwaji wao ndio wauliwaji bora chini ya mbingu. Amesema vilevile kwamba wao ni mijibwa ya Motoni na kwamba wanasoma Qur-aan na haivuki katika koo zao na kwamba wanatoka katika Dini kama jinsi mshale unavotoka kwenye upinde wake na kuwa hawarudi mpaka mshale urudi kwenye upinde wake. Amewaita kuwa ni “mijibwa ya Motoni” na kueleza kuwa hujitokeza katika kila karne; kila wakati inapojitokeza inakatika mpaka atapojitokeza kati yao ad-Dajjaal. Amesema miongoni mwa mambo:

“Mtazidharau Swalah zenu mkizilinganisha na za kwao na Swawm zenu mkizilinganisha na Swawm zao. Wanasoma Qur-aan na haivuki shingo zao.”

Walimuua ´Aliy na ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Wanawaua Waislamu na kuwaacha washirikina, kama alivyosema mkweli na mwenye kuaminiwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mababu wa watu hawa walimuua ´Uthmaan. Baada ya kukata kichwa cha ´Uthmaan mmoja wao akakanyaga kichwa chake kitwaharifu na kusema:

“Ninaapa kwa Allaah sijui siku yoyote maishani ilio bora kama siku hii!”

Kuhusiana na ´Abur-Rahmaan bin Muljam aliyemuua ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu) alisema:

“Nimetia sumu ncha za mshale huu na una matawi tisa. Matawi yake matatu ni ya Allaah na Mtume Wake na masita ni kwa ajili ya kumchukia ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu).”

[1] Umbali kati ya kidole gumba na kidole kidogo.

[2] Tazama http://www.wanachuoni.com/content/maana-ya-wanachuoni-rabbaaniyyuun#

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://video.dusunnah.com/innovations/al-khawarij/the-correct-islamic-position-towards-isis-shaykh-saalih-as-suhaymee/
  • Imechapishwa: 06/11/2016