Ukumbusho wa kutubia na kuusia


Swali: Wanasema wanasema kuwa inapendeza kumkumbusha mgonjwa kutubia na kuacha wasia. Baadhi ya watu wanasema kuwa jambo hili linahusiana na yale maradhi ya khatari na si yale ya madogomadogo. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Kile ninachoonelea ni kwamba mgonjwa akumbushwe kutubia na kuusia katika hali zote. Kwani kutubia ni jambo limewekwa katika Shari´ah katika nyakati zote. Pia kuusia ni kitu kimewekwa katika Shari´ah. Lakini jambo hilo lifanyike kwa njia isiyomsumbua mgonjwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/71)
  • Imechapishwa: 10/08/2021