Ukumbi wa kuswalia ambao kati yake na msikiti kuna barabara


Swali: Katika kitongoji kimoja kuna ukumbi wa swalah wa wanawake ambapo kati yake na msikiti kuna barabara ambayo magari yanapita. Je, wanawake wakamilishe swalah zao ndani yake?

Jibu: Ikiwa kati yake na msikiti kuna barabara basi wanawake wasiswali ndani yake. Wanazuoni wametofautiana juu ya jambo hili. Lakini salama zaidi wanawake wasiswali ndani yake muda wa kuwa ni nje ya msikiti. Wanatakiwa waswali peke yao na wasimfuate imamu. Ni lazima ukumbi huo uwe ndani ya msikiti.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 10/07/2021