Swali: Nataka nasaha kutoka kwako. Mimi katika nyumba yangu hakuna TV. Lakini hivi sasa watoto wangu wamekuwa wakubwa na wakati fulani wanaiomba na mimi ni mwenye kuichukia sana. Wao hivi sasa wanapoenda kwa familia yangu au ndugu wa mke wangu wanakuwa ni wenye kukimbilia TV kama kwamba ni ngamia ambaye hajaona maji kwa muda wa mwezi mzima. Nimesikia kuwa kuna kompyuta za michezo, kwamba kuna kanda za video za kiislamu na filamu za katuni zinazowaigiza mabingwa na vita vya Salaf. Lakini filamu za katuni si zinaingia katika uharamu wa picha kwa sababu ni mapicha yamechorwa kwa mkono? Unaninasihi nini, ee Shaykh, na hali yenyewe ni kama ilivyotajwa. Nisipoingiza kanda na video nyumbani kwangu nazingatiwa kuwa ni mwenye msimamo mkali? Haya ndio tunayosikia kutoka kwa watu wenye imani dhaifu.

Jibu: Kile ninachoona ni kwamba yule ambaye Allaah amemlinda kutokamana na TV basi yuko katika kheri na kompyuta iliyotajwa na muulizaji ni yenye kumtosheleza. Kwa sababu kompyuta wewe ndiye unaiendesha. Bi maana unachezesha kanda za video unazotaka kutoka katika kila kitu. Ni mamoja iwe katika viumbe vya Allaah (´Azza wa Jall), watu mabingwa na mfano wa hayo. Lakini uhalisia wa mambo ni kwamba mabingwa nawachukia. Kwa sababu mtoto mdogo anapokuwa ni mwenye kuwatazama mabingwa hawa ambao ni watu maalum basi itaingia akilini mwake kwamba hakuna mabingwa wengine katika Uislamu isipokuwa mtu huyu tu, jambo ambalo ni tatizo…

Kuhusu maudhui ya picha hizi sio picha zenye kuonekana. Kwa sababu endapo mtu atatazama kanda hii kwa macho anakuwa si mwenye kuona kitu mpaka aiweke katika kifaa ambacho kinaonyesha picha iliyoko katika kanda hii. Kwa hiyo sioni kuwa inaingia katika maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika Malaika hawaingii nyumba ambayo ndani yake kuna picha.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49) http://binothaimeen.net/content/1122
  • Imechapishwa: 06/10/2018