al-Halabiy amesema:

“Wapo na khaswa wanachuoni wakubwa Saudi Arabia ambao bado ni wenye kumsapoti na kumpendekeza Abul-Hasan na al-Maghraawiy. Je, hivi kweli muuliza au mjibiaji kusema kwa jumla ya kwamba fatwa hii kwa mtazamo huo ya kwamba elimu haichukuliwi kwa mwenye kufanya hivo? Hata kama itakuwa inahusiana na wanachuoni wakubwa? Sitaki kutaja jina lolote, lakini ni majina ya wanachuoni wakubwa ambao hawana mashaka yoyote na ni wenye kujulikana.”

1- Saudi Arabia haina maana ya kwamba watu wote wana ´Aqiydah moja. Kuna Hizbiy aliyejificha, mwingine ni Sunniy ambaye hataki kumgusa yeyote na mwingine ni Salafiy anayezungumza haki maadamu inapelekea katika manufaa.

Tutajie wanachuoni hao ili tuwape nasaha. Sidhanii ya kuwa wale wenye kuwasapoti – hata kama watakuwa ni Salafiyyuun – wamesoma na kufikiwa na khabari ya upotevu wa watu hawa wawili. Haitakiwi kwako kuwatumia kama hoja pindi unajua upotevu walionao watu hawa wawili. Ni juu yako kuwanasihi na kujitenga mbali na mfumo wao.

2- Anayejua jinsi al-Maghraawiy anavyomili kwa Khawaarij kisha akamnasihi anatakiwa pia kuchukuliwa kama al-Maghraawiy. Sijui yeyote kutoka katika Ahl-us-Sunnah wanaojulikana kuwa atatilia shaka kuwazingatia hali kadhalika.

3- Ahl-us-Sunnah walifikia utukufu na mafanikio kwa sababu ya kushikamana na dalili kwa ufahamu wa Salaf. Siwezi kufikiria kuwa yeyote katika wao atampaka mafuta yeyote inapokuja katika dini ya Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Durar an-Najmiyyah fiy Radd-ish-Shubuhaat al-´Aqadiyyah wal-Manhajiyyah, uk. 376
  • Imechapishwa: 18/03/2017