Swali: Ni ipi nasaha yako kwa mwanafunzi ambaye amesoma kwa miaka mingi na ananuia kurudi katika mji wake ambapo kumeenea mapote na watu wa Bid´ah wanaoenda kinyume na Ahl-us-Sunnah?

Jibu: Ukirudi katika mji wako na Allaah amekutunuku elimu na ukaijua haki eneza elimu huko na uwalinganie watu katika dini ya Allaah. Allaah (Jalla wa ´Aala) amesema:

وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ

“… na ili waonye watu wao watakaporejea kwao ili wapate kutahadhari.” (09:122)

Ni wajibu kwako kufanya hivi. Simama kwa kutengeneza, kulingania katika dini ya Allaah na ueneze elimu ya Kishari´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13398
  • Imechapishwa: 26/04/2018