Swali: Ni kipi bora kwa mtu akiingia msikitini akamkuta imamu anaadhini?

Jibu: Bora kwake amuitikie muadhini kisha baada ya hapo aombe anachokitaka na halafu aswali Tahiyyat-ul-Masjid. Isipokuwa baadhi ya wanachuoni wamevua katika hayo kwa yule mwenye kuingia msikitini na mwadhini anaadhini siku ya ijumaa adhaana ya pili. Katika hali hiyo anatakiwa kuswali Tahiyyat-ul-Masjid ili apate kusikia Khutbah. Sababu wametoa ni kwamba kusikiliza Khutbah ni lazima na kuitikia mwadhini sio lazima. Kuchunga jambo la lazima ndio linalotakikana kuliko kuchunga jambo ambalo si la lazima.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 285
  • Imechapishwa: 28/04/2020