Swali: Ni ipi hukumu ya kusherehekea sikukuu ya wapendanao? Sikukuu hiyo inakuwa na nembo ambayo ni moyo mwekundu, uwa lekundu na picha ya dubu nyeupe. Sikukuu hiyo ni ya makafiri wanayoisherehekea.

Jibu: Kuafikiana na makafiri katika sikukuu zao ni jambo la khatari sana. Mtu akisherehekea sikukuu zao, akawapongeza au akawapa zawadi katika sikukuu zao kunakhofiwa juu ya mtu huyu. Shaykh Ibn ´Uthaymiyn amesema:

“Kitendo hichi ni aina moja wapo ya kuwapongeza kwa wao kusujudia msalaba au kunywa pombe. Kwa hiyo pindi mtu anapompongeza ni kama vile anavyompongeza kwa kunywa kwake pombe au akampongeza kwa kusujudia kwake sanamu.”[1]

Tunamuomba Allaah usalama na afya. Usherehekeaji ni aina kubwa ya kuafikiana nao. Ni lazima kwa muislamu kuchukua tahadhari ya kujifananisha na mayahudi na wakristo. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hali yake ya chini kabisa ni uharamu. Vinginevyo udhahiri wake ni ukafiri.”

Kutokana na hayo haijuzu kwa mtu kuafikiana na mayahudi, wakristo na waabudu masanamu katika sikukuu na sherehe zao. Wala haijuzu kwake kuwapa zawadi, kukubali zawadi zao wala kuwapongeza. Matendo yote haya ndani yake kuna ukhatari. Isitoshe ni miongoni mwa Bid´ah na mambo yenye uharamu mkubwa. Kunakhofiwa matendo hayo yakawa ni ukafiri na kuritadi. Tunamuomba Allaah usalama na afya. Ni lazima mtu kutahadhari.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/namna-ya-kutangamana-na-makafiri-katika-krismasi/

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191589#219913
  • Imechapishwa: 22/02/2020