Miongoni mwa faida zinazopatikana katika Hadiyth ya Israa´ na Mi´raaj ni pamoja na:

Pili:

1- Uthibitisho wa Ujuu wa Allaah (´Azza wa Jall). Hilo ni kwa njia zifuatazo:

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisafirishwa kupelekwa kwa Mola Wake (´Azza wa Jall), kisha akavuka tabaka saba za mbingu, wakati alipokuwa akienda na kurudi kati ya Mola Wake na Muusa kila wakati Jibriyl ndiye ambaye alikuwa akimpandisha kwenda kwa Mola Wake (Tabaarak wa Ta´ala). Hapa kuna Radd kwa yule mwenye kupinga kuwepo juu kwa Allaah miongoni mwa Jahmiyyah, Mu´tazilah, Ashaa´irah na wengine.

2- Kumthibitishia maneno Allaah (´Azza wa Jall) kwa njia ya kwamba Yeye (Subhaanah) alimfaradhishia swalah bila ya kuwepo mkati na kati. Hapa kuna Radd kwa yule mwenye kupinga Maneno kwa Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/299)
  • Imechapishwa: 21/05/2020