Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

16- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa kuna mtu alimuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amuusie ambapo akamwambia: “Usighadhibike.” Yule mtu akakariri [kuomba kuusiwa] ambapo akamwambia tena: “Usighadhibike.”

Kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Usighadhibike.”

Bi maana usijiingize katika njia mbalimbali zinazopelekea katika hasira. Hivyo, kila njia miongoni mwa njia ambayo inapelekea katika kukasirika, imekatazwa kuindekeza. Ukiona kitu na wewe unajua fika ndani ya nafsi yako kuwa kitakupelekea katika kukasirika, Hadiyth inafahamisha kwamba ukomeke nacho tokea mwanzo na usikiendekeze na hatimaye ukakasirika na pengine ukashindwa kuzima hasira zako.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 252-253
  • Imechapishwa: 14/05/2020