Ujira unabaki kwa aliyejenga msikiti unapobomolewa?

Swali: Msikiti unapobomolewa bado kunabaki ujira wa aliyejitolea kuujenga mara ya kwanza au unaenda (ujira wake)?

Jibu: Kwa kiasi ambacho ´amali yake itakuwa imebaki. Ikiwa kumebaki ´amali yoyote katika msikiti huo, atapata ujira wake kwa kiasi cha hiyo ´amali. Ama ikiwa ´amali yake imeenda na hapakubaki kitu, ´amali yake itakuwa imekwisha na ana yale aliyotanguliza Alhamdulillaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13694
  • Imechapishwa: 20/09/2020