Ibn Baaz kuhusu ujinga ni udhuru III

Swali: Baadhi ya wanachuoni wanasema kuwa watu wa shambani wanaweza kupewa udhuru. Ni mambo yepi wanayoweza kupewa udhuru kwayo au jambo hili lilikuwa ni maalum kwa watu wa zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwanzoni mwa Uislamu?

Jibu: Mtu wa shamba au mwengine anaweza kupewa udhuru kwa kitu kinachowezekana kutokijua. Kwa mfano baadhi ya mambo ya nguzo za swalah, nguzo za zakaah na baadhi ya mambo yanayofuturisha. Ama akipinga uwajibu wa swalah na akasema kuwa hakuna kuswali au akapinga uwajibu wa kufunga Ramadhaan na akasema kuwa hakuna kufunga hapewi udhuru. Haya ni yanayojulikana katika Uislamu fika. Waislamu wote wanayajua haya. Kwa mfano baadhi ya matendo ya hajj yanaweza kufichikana kwake. Lakini hata hivyo haiwezi kufichikana kwake ya kwamba hajj imewekwa katika Shari´ah. Hapa hapewi udhuru.

Swali: Inasemekana ya kwamba kuna ambao hawajui kuoga janaba. Je, hawa wanapewa udhuru?

Jibu: Ambaye si msomi asiyejua anaweza kupewa udhuru na khaswa wanawake. Lakini afunzwe na wala asikufurishwe.

Swali: Aliyefikiwa na vitabu vilivyopinda na vya Bid´ah anapewa udhuru katika hali hii?

Jibu: Hapana. Hapewi udhuru kwayo. Anaweza kupewa udhuru kwa kitu kilichofichikana naye. Kama mfano baadhi ya mambo ya wajibu katika hajj, ´umrah, swawm na mfano wa hayo ambayo kweli yanaweza kumtatiza.

 

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 91-92
  • Imechapishwa: 17/12/2016