Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema ´Aqiydah yetu na ya manaswara ni moja kwa sababu ya mambo ya kidunia na ya kisiasa?

Jibu: Ninamuomba Allaah kinga kutokana na maneno haya. Sisi na manaswara hatuna ´Aqiydah moja. ´Aqiydah ya Tawhiyd na ya Ibraahiym ni kama ´Aqiydah ya utatu? Hivi kweli mtu anasema hivo kwa sababu ya maslahi ya kidunia? Haijuzu.

Ni kweli kuwa inafaa kwetu kufanya biashara nao na kuwa na mikataba na wao katika mambo ya manufaa, na yasioidhuru dini yetu wala sisi hatuko na shari yao. Hata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa na mikataba nao. Hata hivyo haijuzu kwetu kuridhia na kusifu dini yao. Huku ni kumkufuru Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir_27-07-1433.mp3
  • Imechapishwa: 22/05/2018