Uislamu hauna lolote kuhusiana na Qaadiyaaniyyah

Qaadiyaaniyyah bila ya shaka wanadai Uislamu, hata kama Uislamu uko mbali na hauna lolote na wao. Kwa kuwa wamekwenda kinyume na Waislamu katika mambo ya ´Aqiydah. Kwa mfano wanaamini kwamba utume bado haujafungwa. Limethibitishwa hilo kwa Mtume wao Mirzaa Ghulaam Ahmad na wanatukufurisha sisi Waislamu kwa kuwa hatumuamini Mtume wao huyu Dajjaal. Je, hawaamini Kauli ya Allaah (Ta´ala):

وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ

“… lakini ni Mtume wa Allaah na ni mwisho wa Manabii.” (33:40)

Wanaamini. Lau wangeliikanusha wangelikufuru na kuritadi. Vipi basi wataamini andiko hili la Qur-aan na wakati huo huo wanaamini pia kwamba kutakuja Mitume wengine baada ya Mtume wao? Sikilizeni jinsi wameshikamana na Aayah hii na jinsi wamekwenda kinyume na njia ya waumini. Wanasema:

“Nyinyi mmefahamu Aayah hii kimakosa na kwa ajili hiyo mmetumbukia katika makosa na upotevu. Mmefahamu kuwa:

وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ

“… ni mwisho wa Manabii.” (33:40)

ina maana “mwisho wa Manabii.” Hili ni kosa. Ufahamu sahihi wa Aayah ni:

وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ

“… ni mwisho wa Manabii.” (33:40)

Maana yake ni pambo la pete.”

Hivyo, wao wameamini Aayah hii lakini wamekufuru maana yake. Haikuwafaa kitu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://darulhadith.com/islam-har-inget-med-qadiyaniyyah-att-gora/
  • Imechapishwa: 04/09/2020