Swali: Kuna mtu anasema kuwa baadhi ya hukumu za Kishari´ah zinahitajia kutazamwa tena vizuri na kwamba zinahitaji kurekebishwa kwa sababu haziendani na maendeleo ya leo. Mfano wa mirathi kwamba mwanamume kupata mafungu ya wanawake wawili. Ni ipi hukumu ya Shari´ah kwa anayesema mfano wa maneno kama haya?

Jibu: Hukumu zilizowekwa Shari´ah na Allaah katika juu ya waja Wake na akazibainisha katika Kitabu Chake kitukufu au kupitia kwa Mtume Wake mwaminifu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama mfano wa hukumu za mirathi, swalah vipindi vitano, zakaah, swawm na mfano wazo miongoni mwa ambazo Allaah amewawekea nazo wazi waja Wake na Ummah ukaafikiana juu yazo Ummah hautakiwi kupingana nazo wala kuzibadilisha. Kwa sababu ni Shari´ah waliowekewa Ummah katika wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baada ya kufa kwake mpaka Qiyaamah kisimame. Miongoni mwa hukumu hizo ni kufadhilishwa mtoto wa kivulana juu ya mtoto wa kisichana  na watoto na watoto wa kivulana na ndugu wa wazazi na wa baba. Kwa sababu Allaah (Subhaanah) ameliweka wazi katika Kitabu Chake kitukufu na wanachuoni wa waislamu wakaafikiana juu yake. Kwa hivyo ni lazima kuyafanyia kazi kwa kuyaitakidi na kwa kuyaamini.

Yule mwenye kudai kwamba vyema zaidi ni kinyume na hivo ni kafiri. Vivyo hivyo yule mwenye kujuzisha anazingatiwa ni kafiri. Kwa sababu ni mwenye kupingana na Allaah (Subhaanah), Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maafikiano ya Ummah. Ni lazima kwa mtawala kumtaka atubie akiwa ni muislamu. Akitubia, ni sawa, vinginevyo ni lazima kumuua hali ya kuwa ni mwenye kuritadi kutoka nje ya Uislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kubadilisha dini yake muueni.”

Tunamuomba Allaah atusalimishe sisi na waislamu wote kutokamana na fitina zenye kupotosha na kwenda kinyume na Shari´ah safi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/415) https://binbaz.org.sa/fatwas/935/%D8%A7%D9%84%D8%B1%D8%AF-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D9%85%D9%86-%D9%8A%D8%B9%D8%AA%D8%A8%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%AD%D9%83%D8%A7%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B4%D8%B1%D8%B9%D9%8A%D8%A9-%D8%BA%D9%8A%D8%B1-%D9%85%D8%AA%D9%86%D8%A7%D8%B3%D8%A8%D8%A9-%D9%85%D8%B9-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D8%B5%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%AD%D8%A7%D8%B6%D8%B1
  • Imechapishwa: 11/12/2019