Swali: Ni kipi bora adhaana au uimamu?

Jibu: Kuna tofauti juu ya masuala haya. Maoni sahihi ni kwamba adhaana ndio bora kuliko uimamu kutokana na zile Hadiyth zinazofahamisha juu ya fadhilah zake. Kwa mfano maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Lau watu wasingelijua kinachopatikana katika wito na safu ya kwanza kisha wasipate jambo hilo isipokuwa kwa njia ya kupiga kura, basi wangelipiga kura.”[1]

“Waadhini ndio watu wataokuwa na shingo ndefu siku ya Qiyaamah.”[2]

Pengine mtu akasema kuwa uimamu umefungamanishwa na sifa za Shari´ah, kama mfano wa:

“Awaongoze watu yule ambaye ni msomi zaidi wa Kitabu cha Allaah.”[3]

Ni jambo linalotambulika kwamba ambaye ni msomi zaidi ndiye mbora, kitu ambacho kinajulisha kwamba uimamu ni bora kuliko uadhini. Hakika sisi hatusema kuwa hakuna fadhilah katika uimamu – na kitu kina fadhilah – lakini uadhini ni bora kuliko uimamu kwa sababu ndani yake kuna kutangaza utajo wa Allaah (Ta´ala) na kuwazindua watu katika njia ya ujumla. Aidha kazi ya uadhini ni ngumu zaidi kuliko ya uimamu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na makhaliyfah wake waongofu hawakuadhini kwa sababu walikuwa wameshughulishwa na mambo ambayo ni muhimu zaidi. Kiongozi anazingalia hali za watu wote. Lau wangeshughulishwa na kuchungana na wakati basi yangeliwapita mambo muhimu ya waislamu.

[1] al-Bukhaariy (653).

[2] Muslim.

[3] al-Bukhaariy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/159)
  • Imechapishwa: 09/08/2021