Uharamu wa daktari wa kiume kukaa faragha na mgonjwa wa kike

Kwa hali yoyote kukaa faragha na mwanamke wa kando ni jambo ambalo Kishari´ah ni haramu. Haijalishi kitu hata kama ni daktari anayemtibu. Hayo ni kutokana na Hadiyth:

“Mwanamume hakai faragha na mwanamke isipokuwa shaytwaan huwa ni watatu wao.”

Ni lazima aandamane na mwengine pamoja naye. Ni mamoja awe mume wake au mmoja katika Mahram zake wa kiume. Isipowezekana japo mmoja katika ndugu zake wa kike ikiwa hakumpata mmoja katika wale tuliyowataja na wakati huohuo ugonjwa ukawa ni wa khatari usiyoweza kucheleweshwa, basi angalau kwa uchache wahudhurie wauguzi wa kike na mfano wao kwa ajili ya kuzuia faragha iliyokatazwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/13)
  • Imechapishwa: 15/04/2020