Sifa ya maneno imethibiti kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Mu´tazilah wanaona kuwa maneno ya Allaah ni kitu kilichoumbwa na kilichotengana na Allaah. Wanasema kwamba Muusa alisikia maneno ya mti. Jahmiyyah wanayafanya ni maneno yaliyoumbwa na kuachana na Allaah kabisa.

Kuhusiana na Ashaa´irah na Maaturiydiyyah wao wanathibitisha sifa ya maneno. Ni moja katika zile sifa saba wanazothibitisha Ashaa´irah. Ama Maaturiydiyyah ni moja katika zile sifa nane wanazothibitisha. Lakini hata hivyo wanasema kuwa anazungumza kwa maneno yaliyosimama kivyake.

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanatofautiana na wote hao. Wao wanasema kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) anazungumza kwa maneno yenye kusikika yaliyo na Herufi na Sauti. Hakuna kinachosikika isipokuwa tu kile kilicho na herufi na sauti.

Maneno ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) ni sifa Yake ambapo anazungumza pale anapotaka na anazungumza namna anavyotaka. Maneno sio sifa iliyosimama kipekee. Uhakika wa mambo ni kwamba anazungumza kwa sauti inayosikika na wa mbali na wa karibu siku ya Qiyaamah. Sauti yake inaenea kwa malaika walioko mbingu. Sauti yake aliisikia Muusa (´alayhis-Salaam).

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 78
  • Imechapishwa: 27/08/2020