Swali: Yapo makundi kama mfano wa Jamaa´at-ut-Tabliygh na mengineyo. Je, makundi haya ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah? Ni zipi nasaha zako juu ya maudhui haya?

Jibu: Jamaa´at-ut-Tabliygh wako na mambo ambayo ni maovu:

Kwanza mfumo wao umetoka Delhi na haukutoka Makkah wala al-Madiynah. Si vyenginevyo msingi wake ni Delhi huko India. India, kama inavyotambulika, kumejaa ukhurafi mwingi na Bid´ah ingawa kuna Ahl-us-Sunnah wengi ambao wako juu ya Sunnah na juu ya mfumo sahihi. Kama mfano wa kundi la Ahl-ul-Hadiyth ambao ndio watu bora katika nchi hiyo na watu wenye kuigwa katika nchi hiyo. Isipokuwa tu ni kwamba kundi la at-Tabliygh limekulia na limetoka katika nchi hiyo na kutoka katika mji huo na imejengwa juu ya mambo maalum yaliyozuliwa na wale waliozua mfumo huu. Wale waliozua ni Ahl-ul-Bid´ah, wenye kutoka katika Twuruq Suufiyyah na ni miongoni mwa watu waliopinda katika ´Aqiydah. Kwa hiyo ni Bid´ah iliozuliwa. Makundi ulioyakuta katika nchi hiyo ni yenye kutegemea mambo haya yaliyobuniwa na waasisi wa twuruq hizo. Wamepondoka katika ´Aqiydah na katika usulubu wao. Wao ni Suufiyyah. Wao ni Ashaa´irah ambao hawako juu ya mfumo wa Ahl-us-Sunnah, si katika ´Aqiydah wala katika tabia.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 420
  • Imechapishwa: 18/01/2020