Ufafanuzi wa Hadiyth waongo thelathini wenye kudai utume

Swali: Ni yapi makusudio ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakutosimama Qiyaamah mpaka wajitokeze waongo thelathini ambao wote wanadai kuwa ni Mitume.”

Makusudio ni kwamba idadi yao ni thelathini tu au ni zaidi ya hivyo?

Jibu: Idadi yao ni zaidi ya hivyo. Hawa thelathini ni katika wamashuhuri wao. Vinginevyo watajitokeza wengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (12) http://alfawzan.af.org.sa/node/2055
  • Imechapishwa: 15/03/2017