Ufafanuzi kuhusu kumpa nasaha mtawala


Miongoni mwa aina za nasaha kwa mtawala ni kusimama kwa kazi ambayo amembebesha mmoja katika wafanya kazi. Mtu huyo anatakiwa kuisimamisha vizuri, asikhini, asighushi na asiiharibu kazi kwa kufanya mambo yake binafsi ambapo mambo ya waislamu yakaharibika. Huku ni kumfanyia khiyana mtawala. Upande mwengine mtu kusimamia kazi kwa njia inayotakikana hii ndio nasaha kwa mtawala. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mnasihini yule ambaye Allaah amembebesha mambo yenu.”

Miongoni mwa kumfanyia ghushi mtawala ni kule kumsengenya, kumsema vibaya katika vikao, kanda na mimbari. Huku sio kumpa nasaha. Huku ni kumfanyia ghushi na kuwachochea watu katika fitina, kuvuruga umoja na kusababisha uharibifu kwa waislamu. Huku sio kumpa nasaha mtawala.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Masaa´il-il-Jaahiliyyah (02) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/jahlyh_02.mp3
  • Imechapishwa: 22/04/2018