Ufafanuzi bora wa “Kitaab-ut-Tawhiyd” kwa mwanafunzi anayeanza

Swali: Ni ufafanuzi upi bora juu ya “Kitaab-ut-Tawhiyd” kwa mwanafunzi anayeanza?

Jibu: Ufafanuzi bora juu ya “Kitaab-ut-Tawhiyd” cha Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab ni “Fath-ul-Majiyd” cha Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin Hasan. Ni ufupisho wa ufafanuzi wa “Kitaab-ut-Tawhiyd” cha Shaykh Sulaymaan bin ´Abdillaah bin Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, ambacho pia kinaitwa “Taysiyr-ul-´Aziyz al-Hamiyd”. Lakini hakukikamilisha kwa sababu aliuawa. Akaja Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin Hasan ambapo akakifupisha na kukikamilisha kwa kitabu “Fath-ul-Majiyd”. Huu ndio ufafanuzi bora wa “Kitaab-ut-Tawhiyd”.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ al-Maftuuh fiy Masjid Qubaa’ http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17626
  • Imechapishwa: 20/02/2018