Udhhiyah na wanandugu watatu wanaoishi pamoja


Swali: Kuna ndugu watatu wanaishi katika nyumba moja. Kila mmoja katika wao anapata mshahara na amekwishaoa. Je, anawatosha Udhhiyah mmoja au kila mmoja anatakiwa kuchinja kichinjwa chake?

Jibu: Ikiwa chakula chao wote ni kimoja na wanakula pamoja basi kichinjwa kimoja kinawatosha. Yule mkubwa katika wao achinje kwa ajili yake na wale walio nyumbani kwake.

Ama ikiwa kila mmoja ana chakula chake maalum au kwa msemo mwingine anapika kivyake yeye mwenyewe, basi katika hali hii kila mmoja katika wao anatakiwa kuchinja. Kwa sababu hakuna yeyote aliyeshirikiana na mwingine katika chakula na kinywaji chake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (25/42)
  • Imechapishwa: 20/08/2018